Dj Rasmi wa msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Diamond Platinumz, Romy Jons `RJ` amesema kuwa kitendo cha yeye kuwasiliana na Wema Sepetu na kukutana pamoja katika matamasha mbalimbali na hata sherehe haihusiani kabisa na maisha yake baina ya mastaa hao wawili.
Romy amesema kuwa bifu hilo ambalo lilikuwa likiandikwa kwamba hawaelewani tena na Diamond Platinumz kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii na hata magazeti ni kwamba hizo zilikuwa tu njia za watu kuweza kuwagombanisha ndugu hao wawili na wao hawakuwa wakizungumzia swala hilo kutokana na kuchukulia kama kitu cha kawaida.
Akizungumza kwenye mahojiano na Lil Ommy kupitia kipindi cha The Playlist kinachorushwa na kituo cha Redio cha Times Fm Jons ameleeza kuwa yeye hana matatizo na Diamond na hata kuhusu Wema Spetu kuhudhuria kwenye siku yake ya Kuzaliwa na Nasib kutokushiriki yeye halimpi tatizo swala hilo kwa kuwa yeye hajagombana na mtu na kama wao wamegombana haimlazimu na yeye kuingia kwenye kesi hiyo.
“Wamegombana wao, kama wao hawaongei hawakutani hawana umoja sio kwamba ndio inizuie mimi kutokuweza kushirikiana na Wema Sepetu kiuhalisia sio kitu kizuri kufuata hisia za mtu mwingine na hata Diamond kutokuhudhuria kwenye siku yangu ya kuzaliwa haimaanishi kwamba kanichunia kisa Wema alikuja,” alisema.
Akiongelea kuhusiana na yeye kufanya muziki wa Rap kipindi kile, RJ ameeleza kuwa hakuwa na malengo yeyote na muziki alikuwa akifanya kwa vile anapenda sana kuishi maisha ya muziki ila ana kipaji cha kuandika mistari ya na akaifanyia Hip Hop.
“Kipindi kile nilikuwa nafanya muziki kwa kuwa nilikuwa nina passion au niseme love na muziki, nilikuwa napena sana kuishi maisha ya muziki lakini nina kipaji kwenye kuandika mistari na nikiipeleka kwenye upande wa Hip Hop inakuwa mikali sana,” alisema Romy Jons
Kwa upande wa baadhi ya Show za Diamond Platinumz kufanya show katika nchi tofauti na yeye kutokuhudhuria katika show hizo na ukizingatia yeye ndio DJ rasmi, Romy amesema kuwa huwa kunakuwa na baadhi ya maDj ambao wapo kule wakiziba pengo hilo, lakini Pia Diamond ana Crew kubwa sana na sio katika kila matamasha yote wanaenda humo.

