test

Jumapili, 4 Septemba 2016

Bao la Iheanacho lailaza Tanzania



Image captionWachezaji wa Taifa Stars ya Tanzania

Nyota ya Kelechi Iheanacho inaendelea kung'aa ,kwani wiki moja tu baada ya kutia saini kandarasi ya malipo ya pauni 85,000 kwa wiki na kuwa mchezaji anayelipwa juu zaidi nchini Nigeria ameonyesha umahiri wake.

Bao la mda wa ziada la mshambuliaji huyo wa Manchester City ndilo lililoweza kubaini mbivu na mbichi dhidi ya Tanzania katika mchuano wa kufuzu kwa kombe la bara Afrika 2017.
Kutoka kwa kona fupi,mshambuliaji huyo alijitafutia mwanya akiwa karibu na lango la Tanzania star na kuwachilia mkwaju uliopiga mwamba wa goli na kumwacha kipa wa Tanzania bila jibu.

Iheanacho
Image captionIheanacho

Mechi hiyo iliochezwa katika uwanja wa kimataifa wa Akwa Ibom mjini Uyo ilikuwa lazima kwa Nigeria kupata ushindi chini ya Genort Rohr.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx